RC DODOMA AKAGUA MIRADI YA ELIMU KATIKA SHULE YA MSINGI MAYAMAYA, AAGIZA WANAFUNZI WOTE KUREJEA SHULENI

 
































Na Mwandishi wetu
Habari - DODOMA RS 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, tarehe 14, Januari 2026 amefanya ziara ya kikazi katika Shule ya Msingi Mayamaya iliyopo Wilayani Bahi kwa lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya miundombinu ya elimu.

Akiwa shuleni hapo, Mhe. Senyamule amesisitiza wajibu wa watendaji wa kata na vijiji kuhakikisha kuwa ndani ya wiki hii wanafunzi wote wanarejea shuleni kuendelea na masomo yao.

“Ninaagiza watendaji wa kata na vijiji kupita kaya kwa kaya kuhakikisha kila mwanafunzi anarejea shuleni. Hatupaswi kuwa na mtoto anayebaki nyumbani wakati wenzake wakiendelea na masomo, kwani hali hiyo inarudisha nyuma maendeleo ya elimu,” alisema Mhe. Senyamule.

Kwa upande wake  Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mhe. Joachim Nyingo, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa uwekezaji mkubwa alioufanya katika Mkoa wa Dodoma, hususan Wilaya ya Bahi na Kata ya Zanka, unaolenga kuboresha sekta ya elimu na maendeleo kwa ujumla.

Naye  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Bi. Albina Mtumbuka, amesema kuwa Shule ya Msingi Mayamaya imepokea jumla ya shilingi milioni mia tatu na laki mbili kwa ajili ya ujenzi na ukamilishaji wa miundombinu ya elimu. Fedha hizo zilipokelewa tarehe 1 Mei 2025.

Ameeleza kuwa fedha hizo zimetumika kujenga jengo moja la utawala, vyumba sita vya madarasa ya elimu ya msingi, vyumba viwili vya madarasa ya elimu ya awali, pamoja na matundu 12 ya vyoo vya elimu ya msingi na matundu sita ya vyoo vya elimu ya awali.

Aidha, Mbunge wa Jimbo la Bahi, Mhe. Kenneth Ernest Nollo, amewahimiza Wananchi kujenga utamaduni wa kushukuru kwa juhudi na huduma wanazoendelea kupata kutoka Serikalini katika kuboresha sekta ya elimu.


#dodomafahariyawatanzania
#keroyakowajibuwangu
#kazinaututunasongambele




























Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WA HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO

‘WANAWAKE NA SAMIA’ 3000 MKOA WA DODOMA KUPATA MAFUNZO VETA

KAMATI YA USALAMA MKOA WA DODOMA YAFANYA ZIARA PORI LA AKIBA MKUNGUNERO, KONDOA