WAZIRI WA AFYA (MALAWI) NA UJUMBE WAKE WAFIKA DODOMA KUJIFUNZA UTEKELEZAJI WA M-MAMA

 


Ujumbe kutoka nchini Malawi ukiongozwa na Waziri wa Afya wa nchi hiyo Mhe. Madalitso Baloyi wakiwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule kwa lengo la kujitambulisha kabla ya kuanza ziara kuelekea Zahanati ya Chalinze Wilayani Chamwino, Januari 14, 2026, wkwa ajili ya kujifunza utekelezaji wa Mpango wa dharura wa kuokoa maisha ya kina mama wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) ikiwa ni siku ya pili ya ziara yao Nchini, katika Mkoa wa  Dodoma.






Waziri wa Afya wa Malawi Mhe. Madalitso Baloyi na Ujumbe wake wakiwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule kwa lengo la kujitambulisha kabla ya kuanza ziara kuelekea Zahanati ya Chalinze Wilayani Chamwino, Januari 14, 2026, kwa ajili ya kujifunza utekelezaji wa Mpango wa dharura wa kuokoa maisha ya kina mama wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) ikiwa ni siku ya pili ya ziara yao Nchini, katika Mkoa wa  Dodoma.






Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akizungumza na Waziri wa Malawi Mhe. Madalitso Baloyi alipofika ofisini kwake Jijini Dodoma na ujumbe wake kwa lengo la kujitambulisha kabla ya kuanza ziara kuelekea Zahanati ya Chalinze Wilayani Chamwino, Januari 14, 2026, kwa ajili ya kujifunza utekelezaji wa Mpango wa dharura wa kuokoa maisha ya kina mama wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) ikiwa ni siku ya pili ya ziara yao Nchini, katika Mkoa wa  Dodoma.






Baadhi ya wajumbe alioongazana nao Waziri wa Afya wa Malawi wakiwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule kwa lengo la kujitambulisha kabla ya kuanza ziara kuelekea Zahanati ya Chalinze Wilayani Chamwino, Januari 14, 2026, kwa ajili ya kujifunza utekelezaji wa Mpango wa dharura wa kuokoa maisha ya kina mama wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) ikiwa ni siku ya pili ya ziara yao Nchini, katika Mkoa wa  Dodoma.






Waziri wa Afya wa Malawi Mhe. Madalitso Baloyi akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule alipofika ofisini kwake Jijini Dodoma kwa lengo la kujitambulisha kabla ya kuanza ziara kuelekea Zahanati ya Chalinze Wilayani Chamwino, Januari 14, 2026, kwa ajili ya kujifunza utekelezaji wa Mpango wa dharura wa kuokoa maisha ya kina mama wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) ikiwa ni siku ya pili ya ziara yao Nchini, katika Mkoa wa  Dodoma.






Waziri wa Afya wa Malawi Mhe. Madalitso Baloyi (kulia)  na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule katika picha ya pamoja baada ya kufika ofisini kwake Jijini Dodoma kwa lengo la kujitambulisha kabla ya kuanza ziara kuelekea Zahanati ya Chalinze Wilayani Chamwino, Januari 14, 2026, kwa ajili ya kujifunza utekelezaji wa Mpango wa dharura wa kuokoa maisha ya kina mama wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) ikiwa ni siku ya pili ya ziara yao Nchini, katika Mkoa wa  Dodoma.






Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule (kulia) akiwa na mmoja wa ujumbe ulioongozana na Waziri wa Afya wa Malawi walipofika ofisini kwake Jijini Dodoma kwa lengo la kujitambulisha kabla ya kuanza ziara kuelekea Zahanati ya Chalinze Wilayani Chamwino, Januari 14, 2026, kwa ajili ya kujifunza utekelezaji wa Mpango wa dharura wa kuokoa maisha ya kina mama wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) ikiwa ni siku ya pili ya ziara yao Nchini, katika Mkoa wa  Dodoma.






Waziri wa Afya wa Malawi Mhe. Madalitso Baloyi na Ujumbe wake wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule baada ya kufika ofisini kwake Jijini Dodoma kwa lengo la kujitambulisha kabla ya kuanza ziara kuelekea Zahanati ya Chalinze Wilayani Chamwino, Januari 14, 2026, kwa ajili ya kujifunza utekelezaji wa Mpango wa dharura wa kuokoa maisha ya kina mama wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) ikiwa ni siku ya pili ya ziara yao Nchini, katika Mkoa wa  Dodoma.






Baadhi ya Viongozi walioongozana na Waziri wa Afya wa Malawi Mhe. Madalitso Baloyi wakiwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chamwino kwa lengo la kujitambulisha kabla ya kuelekea Zahanati ya Chalinze Wilayani humo kwa ajili ya kujifunza utekelezaji wa Mpango wa dharura wa kuokoa maisha ya kina mama wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) ikiwa ni siku ya pili ya ziara yao Nchini, katika Mkoa wa  Dodoma Januari 14, 2026.






Waziri wa Afya wa Malawi Mhe. Madalitso Baloyi akizungumza na Watumishi wa Zahanati ya Chalinze Wilayani Chamwino pamoja na wananchi wa Kata ya Manchali wakati wa ziara yake aliyoambatana na Ujumbe wake kwa ajili ya kujifunza utekelezaji wa Mpango wa dharura wa kuokoa maisha ya kina mama wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) ikiwa ni siku ya pili ya ziara yao Nchini, katika Mkoa wa  Dodoma Januari 14, 2026.














Baadhi ya Watumishi wa Zahanati ya Chalinze Wilayani Chamwino, Ujumbe kutoka Malawi na wananchi wa Kata ya Manchali wakimsikiliza Waziri wa Afya wa Malawi  Mhe. Madalitso Baloyi wakati wa ziara yake iliyolenga kujifunza utekelezaji wa Mpango wa dharura wa kuokoa maisha ya kina mama wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) katika Zahanati hiyo ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake Nchini, katika Mkoa wa  Dodoma Januari 14, 2026.







Baadhi ya kina mama ambao pia ni wanufaika wa Mpango wa M-MAMA wakitoa ushuhuda wakati wa ziara ya Waziri wa Afya wa Malawi Mhe. Madalitso Baloyi aliyoambatana na Ujumbe wake kwa ajili ya kujifunza utekelezaji wa Mpango wa dharura wa kuokoa maisha ya kina mama wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) ikiwa ni siku ya pili ya ziara yao Nchini, katika Mkoa wa  Dodoma Januari 14, 2026.






Waziri wa Afya wa Malawi Mhe. Madalitso Baloyi katika picha ya pamoja na kina mama wanufaika wa Mpango wa M-MAMA wakati wa ziara aliyoambatana na Ujumbe wake kwa ajili ya kujifunza utekelezaji wa Mpango wa dharura wa kuokoa maisha ya kina mama wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) ikiwa ni siku ya pili ya ziara yao Nchini, katika Mkoa wa  Dodoma Januari 14, 2026.






Na Mwandishi wetu – DODOMA RS

Waziri wa Afya wa nchini Malawi Mhe. Madalitso Baloyi akiambatana na ujumbe wake, Januari 14, 2026, wamefanya ziara kwenye Zahanati ya Chalinze, Wilaya ya Chamwino inayolenga kujifunza namna Mpango wa dharura wa kuokoa maisha ya kina mama wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) unavyofanya kazi ikiwa ni siku ya pili ya ziara yao Nchini, katika Mkoa wa  Dodoma.

Akiwasilisha taarifa ya faida za Mpango huo, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Eusebi C. Kessy, amesema tangu kuanza rasmi kwa M-MAMA 2022, umesaidia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwani mwaka 2025, kulikua na jumla ya vizazi 17,740 kutoka kwenye vituo vyote 82 vya kutolea huduma huku kukitokea vifo 3 vya kina mama na 12 vya watoto wachanga ukilinganisha na mwaka 2024 ambapo kulitokea vifo 5 vya kina mama na 20 vya watoto wachanga.

Wakiwa katika Zahanati hiyo, wamepata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na jinsi huduma hiyo inavyofanya kazi na kusaidia kina mama na watoto wachanga kwa kusikia shuhuda za kina mama na madereva wanaofanya safari hizo za dharura.

Waziri huyo amesema; “Mimi na timu yangu tumekuja kujifunza hiki mnachokifanya.Kwa Malawi bado hatujaanza kusafirisha wagonjwa, lakini tumeshaanza kutekeleza, haya tuliyojifunza hapa, tutakwenda kuyatekeleza kule kwetu kwa kuwa lengo hapa ni kuokoa maisha”. Mhe. Baloyi

Kadhalika, mmoja wa wanufaika wa Mpango huo Bi. Elizabeth Daniel, amesema mwaka 2024, alijifungua watoto mapacha kabla ya muda wa kujifungua, katika Zahanati hiyo ambapo alipatiwa rufaa kupitia Mpango huo na kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa na kupata huduma bora.

Vile vile, Dereva Jamii wa M-MAMA MwalimuYustus H. Uledi, amesema anaifanya kazi hiyo kwa kujitolea na si kama biashara inayolenga faida na anajivunia kwani ni kazi inayo okoa maisha ya Mama na Mtoto na kutoa wito kuwa kina mama na watoto wachanga wanahitaji msaada zaidi.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wananchi wa Kata ya Manchali, Diwani wa Kata hiyo, Mhe. Nasson M. Mtundu amesema Serikali ina mpango wa kujenga kituo cha afya kwenye Kata yake yenye vijiji vitano ambacho kitasaidia kuboresha zaidi huduma za uzazi kwa wananchi wake.

Awali, ugeni huo ulifika kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule kujitambulisha na kuelezea lengo la ziara ambapo Mhe. Senyamule alisema M-MAMA imekua msaada mkubwa katika kuokoa maisha ya kina mama na watoto wachanga na imepunguza kwa kiasi kikubwa vifo vya uzazi.

Mpango wa M-MAMA ulizinduliwa rasmi katika Mkoa wa Dodoma Agosti 11, 2022 na kuanza kutumika Novemba 18, 2022 baada ya kufanya mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na kuwatambua madereva jamii, kuwapatia mafunzo, kuwasajili kwenye mfumo pamoja na kutoa mafunzo kwa watumishi juu ya kutambua dalili za hatari mapema kwa mama mjamzito na mtoto mchanga na kuwasambazia nyaraka za rufaa.



#DodomaTunatakaAmani
#AmaniYetuUstawiwetu
#WekezaDodomaStawishaDodoma
#KazinaUtuTunasongaMbele





































Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WA HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO

‘WANAWAKE NA SAMIA’ 3000 MKOA WA DODOMA KUPATA MAFUNZO VETA

KAMATI YA USALAMA MKOA WA DODOMA YAFANYA ZIARA PORI LA AKIBA MKUNGUNERO, KONDOA