TBS YATOA VYETI 29 VYA UBORA KANDA YA KATI
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Senga Gugu amewatunuku Vyeti na Leseni wafanyabiashara na wazalishaji ambao bidhaa zao zimethibitishwa Ubora wake na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa wazalishaji wa kanda ya kati (Dodoma, singida na Tabora) pamoja na Iringa na kuwaasa wazalishaji kuhakikisha bidhaa zote zinazozalishwa viwandani zinazingatia kanuni bora za uzalishaji. Hafla hiyo imefanyika leo tarehe Aprili 28,2023 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma. "Kazi hii iliyofanywa na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, kupitia TBS ni mwendelezo wa azma ya Serikali katika kuhakikisha wazalishaji wa bidhaa viwandani kama wadau muhimu wa maendeleo ya ubora na usalama wa bidhaa, wanazalisha bidhaa zinazokidhi matakwa ya Viwango vya ubora Kitaifa na kimataifa na kuhakikisha Watanzania wananunua na kutumia bidhaa zenye ubora na ambazo ni salama kwa afya zao na mazingira "Nitoe rai kwenu nyote ambao mmeshiriki kutimiza waji...