Posts

Showing posts from June, 2023
Image
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule amemtembelea na kumjulia Hali Bi. Witness Mkuvalwa (mkazi wa Iringa) anayesadikiwa kumwagiwa kimiminika chenye kemikali na kulazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa Uangalizi na Matibabu. Senyamule amemtembelea Bi. Witness leo Juni 30,2023 na kuahidi kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Mkoa katika kuhakikisha anayetuhumiwa kuhusika na kitendo hicho anachukuliwa hatua na majeruhi wa tukio hilo anapata haki yake. Kwa Mujibu wa Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo Dkt. Baraka Mponda amekiri kumpokea Bi.Witness Mkuvalwa jumatano ya Juni 28 mwaka huu ambapo tukio la kumwagiwa kimiminika hicho lilitokea katika Stendi kuu ya Mabasi ya Nanenane Jijini Dodoma. Katika kuhahikikisha Bi. Witness anarejea katika hali yake ya kawaida Madaktari Bingwa wa Macho,Pua, Koo na Ngozi wamempima mgonjwa huyo na kuthibitisha hakupata madhara Makubwa hivyo ataendelea vizuri kutokana na Matibabu anayopatiwa. Mhe.Senyamule pia alipata fursa ya kuwate...
Image
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Joyce Ndalichako amempongeza Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Mhe. Khadija Taya (Keisha) kwa kuandaa Chakula Cha Mchana kwaajili ya watu Wenye mahitaji Maalumu katika Mkoa wa Dodoma. Pongezi hizo zimetolewa katika Hafla ya chakula hicho iliyofanyika leo tarehe 28/06/2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma Jengo la Mkapa ambapo amekiri Serikali kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuboresha Mahusiano mazuri na Watu Wenye mahitaji Maalumu. "Kwa hakika hili ni Jambo kubwa linaloonyesha upendo na namna ambayo unawathamini watu wenye mahitaji Maalum na kaulimbiu ya 'upendo kwa watu Wenye Ulemavu ni upendo kwa jamii nzima' hii ni kaulimbiu ambayo inatukumbusha wanajamii wote kuwakumbuka watu Wenye mahitaji Maalumu nakupongeza sana kwa Jambo hili",Amesema Ndalichako. Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule amesema kati ya wakazi milioni 3 wa Mkoa huo...

KAMPUNI YA DOYCARE YAWASITIRI WANAFUNZI WA KIKE DODOMA

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amepokea boksi 84 za taulo za kike kutoka kwa kampuni ya Doy Care ambao watengenezaji na wasambazaji wa taulo hizo kwa ajili ya kuratibu ugawaji kwa wanafunzi wa Shule mbalimbali katika Mkoa wa Dodoma. Akipokea taulo hizo Mhe. Senyamule ameishukuru Kampuni hiyo kwa msaada wa taulo hizo ambazo zinaenda kusaidia watoto wa kike kuwasitiri na kuwezesha kuhudhuria masomo bila kikwazo chochote. “Ninawashukuru sana kwa kujali makundi yenye uhitaji, ni mchango mkubwa kwa Mkoa wa Dodoma hususan kwa wazazi ambao hawana uwezo wa kuwezesha ununuzi wa taulo za kike. Tutahakikisha tunawapa walengwa ambao ndio wahitaji hasa wenye mazingira magumu.” Senyamule amesisitiza. Amesema atawasisitiza wanafunzi wanaufaika wa taulo hizo kusoma kwa bidii ili kazi inayofanywa na kampuni ya kusambaza taulo hizo iwe na manufaa na kuonyesha kuwa msingi mkubwa ni wao kupata elimu. Nae Afisa Taaluma Mkoa wa Dodoma Bi. Jane Mangowi amesema taulo hizo pia zitasaidia wanafu...

UONGOZI WA VODACOM WAMTEMBELEA RC-SENYAMULE

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amekutana na kufanya mazungumzo na Watendaji wa Vodacom Tanzania waliofika Ofisini kwake leo Juni 27, 2023 kwa lengo la kujitambulisha na kuimarisha uhusiano uliopo baina yao na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika utoaji wa huduma kwa wananchi na kuchangia katika Maendeleo ya Mkoa wa Dodoma na Taifa kwa ujumla.  Katika mazungumzo yao Kampuni ya Vodacom Tanzania Ltd imelenga pia kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa katika kutoa huduma bora kwa wateja kwa kuandaa mfumo uliounganika wa kutoa huduma hizo ili kuwezesha upatikanaji rahisi wa takwimu. Ugeni huo umeongozwa na Bw. Philip Besiimire Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Bi.Zuweina Farah Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano Vodacom Tanzania na Bi. Grace Lyon Meneja Mahusiano ya Serikali Vodacom Tanzania. MWISHO  

SENYAMULE ARIDHISHWA NA UJENZI MNARA WA MASHUJAA

Image
 Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amekagua na kuridhishwa na Kasi ya Ujenzi wa Mnara wa Mashujaa unaojengwa katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma kwa dhamira ya kuwaenzi Mashujaa mbalimbali waliopigania Taifa la Tanzania. Senyamule amefanya ukaguzi huo Leo Tarehe 26/06/2023 ikiwa ni ziara ya kikazi ya Maandalizi ya siku ya Mashujaa Nchini inayotarajiwa kudhimishwa Julai 25,Mwaka huu na Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais waTanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan 

SERIKALI KUENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI DODOMA

Image
  Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kutatua changamoto mbalimbali ndani ya jiji la Dodoma kwa lengo la kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Daniel Chongolo katika viwanja vya Mtekelezo vilivyopo Shule ya Sekondari Central Jijini Dodoma akihitimisha  ya ziara yake ya siku kumi ndani ya Mkoa wa Dodoma. Ndugu Chongolo amesema kuwa changamoto hizo ni pamoja na migogoro ya ardhi, sekta ya kilimo, elimu, Maji na ubovu wa miundombinu ya kufika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya. Ndugu Chongolo amesema kuwa lengo la ziara yake  mkoani humo ni ilikuwa ni kusikiliza wananchi wa Mkoa wa Dodoma na kutatua changamoto zao.   Vile vile amewaasa wafanyakazi wote waliopata nafasi za ajira kwenye miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa kufanya kazi kwa bidii ili kulinda ajira zao pamoja na kuacha tabia ya wizi na kuchukua vitu visivyo halali badala yake...
Image
Uongozi wa shirika la Global Communities Tanzania ulifika ofisi za katibu tawala wa mkoa wa Dodoma Bw Ally Gugu kwa lengo la kuwasilisha na kutambulisha rasmi mradi wa “Pamoja Tuwalishe”.  Mradi huu kwa kushirikiana na serikali, jamii na wadau una lengo la kuimarisha lishe katika shule za awali na msingi ili kuboresha elimu katika wilaya tatu za mkoa wa Dodoma ambazo ni Chemba, Kondoa na Bahi. Ma lengo ya mradi huo ni Kuboresha ujuzi wa wanafunzi; Kuboresha afya na Lishe ya wanafunzi;Kuimarisha mifumo ya utekelezaji wa Muongozo wa chakula na Lishe  shuleni.