
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Gugu amefungua kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mradi ya uboreshaji wa huduma za afya ya uzazi na mtoto kwa Halmashauri ya Mpwapwa kilichofanyika leo tarehe 30 agosti 2023 katika ukumbi wa Hospitali ya Mpwapwa. Akizungumza katika kikao hicho Gugu amesema ni vyema kuzingatia mikakati iliyopo ili miradi ambayo ipo katika Halmashauri inakamilika kwa wakati na kuleta manufaa kwa wananchi. Amesema wataalamu wanatakiwa kuhakikisha miradi inatekelezwa na kusimamia kwa ubora kama serikali ilivyokubaliana na wadau wa KOFIH kwa lengo la kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati kama ilivyokubalika. “Kila Halmashauri ni lazima kuhakikisha vifaa tiba vinanunuliwa kwa wakati na wananchi waweze kuvitumia, kunufaika na kuongeza tija kwa wananchi. “Serikali yetu inatoa kipaumbele kwenye suala la afya hivyo tunaona Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa kipaumbele kwenye suala la afya ya mama na mtoto hiv...