Bodi ya Barabara Mkoa wa Dodoma leo Desemba 20, 2023 imefanya kikao chake cha kwanza mwaka 2023/24 kuwasilisha, kujadili na kushauri juu ya utekelezaji wa miradi ya Barabara za Mkoa kwa kipindi cha Julai hadiNovemba. Kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, kimefanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkoa jengo la Mkapa Jijini Dodoma Katika kikao hicho, Mwenyekiti amewasilisha taarifa ya bajeti ya jumla ya Mkoa kwenye ujenzi wa miundombinu ya Barabara na kuwataka wajumbe kwa niaba ya wananchi kufanya maendeleo ili kuinua Uchumi kulingana na maendeleo yaliyopatikana. "Mkoa umepata jumla ya shilingi Bilioni 230.29 kutekeleza miradi ya Barabara kwa kipindi cha miaka mitatu ambapo TANROADS wamewezeshwa kutengeneza Barabara zenye jumla ya urefu wa Km 9248.12, TARURA wamewezeshwa kutengeneza Barabara zenye urefu wa jumla ya Km 7540.9 ambapo jumla wote wamepatiwa kiasi cha Shilingi Bilioni 593 na Milioni 69. " Utekelezaji huu wa miradi...