Posts

Showing posts from January, 2024

SERIKALI YAANZA UTEKELEZAJI WA UJENZI WA CHUO MAHIRI CHA TEHAMA ENEO LA NALA -DODOMA

Image
Serikali  kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeanza utekelezaji wa ujenzi wa Chuo  Mahiri cha  TEHAMA katika Jiji la Dodoma eneo la Nala . Utekelezaji wa Miradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa tatu wa Taifa wa Maendeleo wa mwaka 2021/2026 na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020/2025 ambayo inasisitiza uwepo wa mafunzo ya Ujuzi na Ubunifu katika TEHAMA nchini. Hayo yamebainishwa na Katibu Makuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,  Mohammed Khamis Abdulla leo Januari 29 Jijini Dodoma katika mkutano na Wanahabari wakati wa kikao cha ufunguzi wa ujenzi wa Chuo Mahiri cha TEHAMA Dodoma kati ya Wizara hiyo na Washauri Elekezi Chuo cha Hanyang kutoka nchini Korea.  Katibu Mkuu huyo amasema Vyuo hivyo vya TEHAMA vitakua kitovu cha taaluma, Ujuzi, ubunifu, Tafiti, Maarifa na kukuza ujasiri amali wa kidijitali Kitaifa na Kimataifa. Ujenzi wa Chuo  hicho cha  TEHAMA utachochea maendeleo katika w...

WANADODOMA MNAKARIBISHWA KUTEMBELEA BANDA LA MAONESHO.

Image
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kitengo cha huduma za kisheria kwa kushiriki na kitengo cha Ofisi ya Kamshina wa ardhi wa Jiji la Dodoma wanawakaribisha wananchi wote wa Mkoa wa Dodoma kupita katika Banda la Mkoa wa Dodoma lililopo katika viwanja vya Nyerere square' ili kujipatia huduma mbalimbali za msaada wa kisheria kutoka kwa mwanasheria wa Mkoa huo Bw. Jofrey Pima. Maonyesho hayo yanafanyika ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Sheria iliyoanza tangu januari 24 na inatarajiwa kutamatika kesho januari 30/2024. Aidha,Huduma zinazotolewa na banda hilo ni pamoja na utoaji wa namba za miamala kwa ajili ya malipo ya hati (control number),kupokea na kutatua changamoto mbalimbali za wateja zinazohusu ardhi,kusajili usajili wa hati na nyaraka za ardhi sambamba na kuelimisha jamii matumizi sahihi ya ardhi. #wiki ya sheria #Dodomafahariyawatanzania ,Wekeza Dodoma, Stawisha Dodoma.
Image
  Wadau wa lishe Mkoa wa Dodoma leo Januari 29, 2024 wamefanya kikao cha  robo ya kwanza ya mwaka kikijadili hali ya upatikanaji wa chakula shuleni kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma. Kikao hicho kimekazia umuhimu wa chakula kwa wanafunzi ikiwa ni nguzo muhimu ya kuinua Taaluma ki Mkoa na muarobaini kwa changamoto za utoro shuleni hasa kipindi hiki ambacho Mkoa umeweka Mkakati wa kuinua taaluma.

MKOA WA DODOMA WAADHIMISHA KIPEKEE SIKU YA KUZALIWA KWA RAIS MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

Image
Mkoa wa Dodoma ukiongozwa na Mhe. Rosemary Senyamule leo Januari 27/2024 umeadhimisha  kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutembelea kituo cha Taifa cha watoto wenye mahitaji maalum cha Samia Suluhu Hassan kilichopo kikombo Jijini Dodoma. Akihutubia Makutano waliojitokeza katika kuadhimisha siku hiyo Mhe. Senyamule amesema Mkoa wa Dodoma unayo mambo mbalimbali ya kujivunia yaliyofanywa na Rais huyo ikiwemo kujengwa Miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoani humo. "Mhe. Rais amebeba majukumu ya pande zote Kama kiongozi, mama na raia namba moja wa Tanzania, leo sisi wanadodoma tunayo Miradi mbalimbali tunayojivunia iliyotokana na utashi na kutupatia Fedha za kutekeleza Miradi hiyo ya maendeleo ambayo inawagusa wananchi moja kwa moja, wanadodoma tunamuombea kheri katika uongozi wake," amesema Senyamule Hata hivyo Mhe. Senyamule amempongeza Rais Samia kwa kuendelea kutenda haki, kuweka vipaumbele kwa Mambo yanayo...
Image
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule ameshiriki uzinduzi wa wiki ya Sheria Nchini uliofanyika leo januari 27/01/2024 katika viwanja vya 'Nyerere square' Jijini Dodoma. Maadhimisho ya wiki ya Sheria Nchini yameanza tangu januari 24 na yanatarajiwa kutamatika ifikapo januari 30/2024 huku Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule ameshiriki uzinduzi wa wiki ya Sheria Nchini uliofanyika leo januari 27/01/2024 katika viwanja vya 'Nyerere square' Jijini Dodoma. Maadhimisho ya wiki ya Sheria Nchini yameanza tangu januari 24 na yanatarajiwa kutamatika ifikapo januari 30/2024 huku kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni "Umuhimu wa Dhana ya haki kwa ustawi wa Taifa : Nafasi ya Mahakama na wadau katika kuboresha mfumo jumuishi wa Haki Jinai". Mgeni rasmi aliyefanya uzinduzi katika maadhimisho hayo ni spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson.kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni "Umuhimu wa Dhana ya haki kwa ustawi wa Taifa : Nafasi ya Mah...

WANANCHI WA DODOMA WAHIMIZWA KUTUNZA MISITU

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewataka wananchi wa Mkoa wa huo hasa wakazi wa Kata ya Zanka Wilayani Bahi kuachana na biashara ya kuuza mkaa na badala yake waanze kujishughulisha na shughuli mbadala  zitakazowaletea kipato ili kutunza misitu wa Hifadhi ya Chenene. Wito huo umetolewa Leo Januari 25,2024 wakati wa ziara yake ya kikazi ya kusikiliza na kutatua kero zao , Ziara hiyo imeenda sambamba na ukaguzi  wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa Wilayani humo.  Miradi hiyo ni ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa kwa kila shule katika shule ya msingi Ibihwa na Mundemu na  matundu 21 shule ya msingi Zanka yenye thamani ya  Shilingi 168,389,815.02. "Nitoe wito wangu kwa wananchi, jaribuni kutafuta shughuli mbadala za kupata kipato cha kukuza uchumi wenu na  kuendelea kutunza mazingira kwani kuna fursa ya Barabara ya Dodoma- Manyara. Tumieni nafasi hii kuji vipato vyetu." Amesisitiza  Mhe. Senyamule  Aidha, amewataka...
Image
  Ziara ya Ukaguzi wa Miradi ya Ujenzi wa Barabara imefanyika katika Wilaya nne za Mkoa wa Dodoma ikiongozwa na Waziri mwenye dhamana ya Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa ,ambapo kwa nyakati tofauti ametembelea Wilaya za Kongwa, Mpwapwa ,Chamwino na Dodoma jiji kujionea hali halisi ya miundombinu ya Barabara katika Wilaya hizo. Ziara hiyo ya Ukaguzi imefanyika ndani ya siku mbili ambapo leo Januari 20 /2024 amehitimisha ndani ya Mkoa huo. Amekagua na kujionea namna wakala wa Barabara Mkoa wa Dodoma (TANROADS) wakiendelea kutatua changamoto ya Maji ya mvua kukata mawasiliano kwa muda pindi mvua zinaponyesha katika kata ya Mtanana Kongwa, Ujenzi wa Barabara wa Km 7.5 Wilayani Mpwapwa na kujionea namna daraja la nzari linavyokwamisha shughuli za maendeleo wananchi hususani katika kipindi cha mvua na Barabara ya mzunguko Kutoka mtumba hadi veyula jijini Dodoma. Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amemshukuru Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya M...