Posts

Showing posts from May, 2024

NMB YADHAMINI UMITASHUMITA DODOMA.

Image
Benki ya NMB kanda ya kati Leo Mei 31/2024 wamekabidhi tracksuit jozi 150 Kwa kaimu afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Bi. Sophia Mbeyu Kwa ajiri ya timu ya Mkoa ya wanafunzi watakaoshiriki  UMITASHUMITA ngazi ya Taifa yanayotarajiwa kuanza juni 5 na kutamatika juni 15 Mkoani Tabora.  Makabidhiano hayo yamefanyika na Kaimu Meneja kanda ya kati Bw. Victor Dilunga katika viwanja vya Shule ya Dodoma Sekondari na kupokelewa na Kaimu afisa Elimu Mkoa Mwl. Sophia Mbeyu.  Hatahivyo Benki hiyo wametoa vifaa hivyo ikiwa ni kurudisha Kwa jamii pamoja na kuwatangazia wanafunzi hao huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa elimu juu ya akaunti ya Chipukizi ya watoto walio na umri wa  miaka 14-17. #NMBkaribuyako #dodomafahariyawatanzia #michezoniafya #umitashumita2024

RUWASA DODOMA KUFIKISHA MAJI VIJIJI KWA 85% IFIKAPO 2025

Image
Wakala wa Maji na Usafiri wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Dodoma umedhamiria kufikisha maji Vijijini kwa asilimia 85 kama inavyosema ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).  Hayo yamebainishwa leo Mei 31, 2024 kwenye kikao cha Watumishi wake wote wa Mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma. Kikao hicho kilichokwenda sambamba na mafunzo kwa Watumishi juu ya namna ya kujiandaa kustaafu Mapema, kimehudhuriwa na Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ambaye amewasihi kutimiza azma hiyo. "Takwimu zinaonesha, kabla ya kuanzishwa RUWASA, maji yalifika Vijijini Mkoa wa Dodoma kwa asilimia 57.4  lakini tangu kuanzishwa kwake, umepanda hadi kufikia 66.3%. Niwapongeze sana. Ilani ya Chama Cha Mapinduzi inataka kufikia 2025, muwe mumefikia 85%. Kutokana na mikakati muliyojiwekea, nina imani mutaweza kufikia lengo". Amesema Mhe. Senyamule  Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya, ambaye alikuwepo kwenye kikao hicho, amesema kuwa...

WAKAZI WA MTERA WAIOMBA SERIKALI KUSHUGHULIKIA ADHA YA MAMBA

Image
Mkuu wa Mkoa wa  Dodoma  Mhe. Rosemary Senyamule amewasihi wakazi wa Kijiji cha Mtera  kuwa wavumilivu wakati mchakato wa Serikali unaendelea kuhusu zoezi la uvunaji  wa Mamba katika bwawa la Mtera kutokana na wanyama hao kusababisha vifo mara kwa mara kwa wakazi wa eneo hilo. Mhe. Senyamule ametoa wito huo Mei 29, 2024 kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Mtera na kuibua kero hiyo ya Mamba na kuomba Serikali iendeshe zoezi la uvunaji wa mamba hao katika kijiji hicho.   Kwa Upande Wake Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar Mmuya amewaelekeza watendaji wa vijiji kuwa wawazi kwa wananchi wao inapotokea Serikali inatekeleza Jambo la maendeleo kwa wananchi kwa kutoa taarifa kwenye mikutano ya hadhara na  kubandika  matangazo sehemu mbalimbali. Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Theopista Mallya amewasihi wakazi wa Mtera kukaa mbali na vitendo viovu kwa kutii Sheria bila shuruti ili kujiepisha na Mkono wa Sheria. Reply Forward Add reaction ...

TAWEN YAZINDULIWA DODOMA

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule Mei 25, ameshiriki uzinduzi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ijulikanayo kama Tanzania Women Empowerment Network (TAWEN) Mkoani humo  ambapo mgeni rasmi katika hafla hiyo ni Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Suleiman Jafo kwenye ukumbi wa mikutano jengo la PSSF . Taasisi ya TAWEN inawasaidia na kuwawezesha wanawake na wasichana kutambua mchango wao na kuthibitisha misingi sawa ya kiuchumi, kiuongozi na kitamaduni katika kutengeneza jamii yenye usawa kimawazo na kimaendeleo. Hatahivyo huduma mbalimbali zinazotolewa na Taasisi hiyo ni pamoja na kutoa taarifa za kibiashara, uandaaji wa makongamano na maonesho, kuwajengea uwezo wanawake kupitia mafunzo mbalimbali, kutoa ushauri wa kibiashara, kufanya utetezi na ushawishi kwa niaba ya wanawake katika masuala ya sera na Sheria mbalimbali na kuwasaidia wanawake kupata masoko yenye uhakika wa bidhaa zao.

MHE. SENYAMULE AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA BIASHARA MKOA

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule  tarehe 24.05.2024 ameongoza kikao cha baraza la biashara la Mkoa huo kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano Jengo la Mkapa. Lengo la kikao hicho ni kujadili masuala la biashara na uwekezaji kikiongozwa na mada mbalimbali ambazo ni  pamoja  na mfumo wa masoko wa kieletroniki, matokeo ya tathmini ya mazingira ya biashara yanayokwamisha ukuaji wa biashara kwa sekta binafsi na wasilisho kuhusu stakabadhi ghalani . Sambamba na hayo kikao hicho kimeazimia mambo kadhaa ikiwamo timu ya watalaam iundwe kwa ajili ya kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo  Mkoa huo na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kuboresha namna  kutoa elimu kwa wafanyabiashara wadogo (machinga) nk. Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar Mmuya amewahimiza wadau wa sekta binafsi na Halmashauri zote za Mkoa huo kufanya uwekezaji katika sekta ya  maliasili na utalii hususani ufugaji wa  nyuki kwani ni ufugaji  wa  muda mf...

WENYEVITI WA BODI NA KAMATI ZA SHULE WATAKIWA KUZUIA UTOVU WA NIDHAMU

Image
Wenyeviti wa bodi na kamati za shule za Msingi na Sekondari Mkoa wa Dodoma, wametakiwa kusimamia nidhamu kwa wanafunzi  kwani matukio mengi ya ukiukwaji wa nidhamu yanapotokea huchukuliwa hatua kuliko jitihada za kuzuia yasitokee. Hayo yamebainishwa leo Mei 17, 2024 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa kikao kazi kilichoitishwa na seksheni ya Elimu Mkoa kwa lengo la kuwajengea uelewa viongozi hao. Kikao hicho kimefanyika kwenye Shule ya Msingi Mtemi Mazengo Jijini Dodoma. Akifungua kikao hicho, Mhe. Senyamule amesema; "Nafahamu jukumu lenu kubwa ni kusimamia nidhamu, lakini hebu muje na mikakati thabiti ya kuzuia tusipate matokeo ya utovu wa nidhamu. Lazima tutumie nguvu nyingi kulinda nidhamu kabla hatujachukua hatua pale inapovunjwa". Amesema Mhe. Senyamule. Hata hivyo, Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Mwl. Vicent Kayombo, amesema kikao hiki ni utekelezaji wa maagizo ya Serikali ya Mkoa ambayo yamelenga kutimiza Mkakati wa Elimu 2024 uliowekwa kwa shabaha y...