PBZ WAMTEMBELEA KATIBU TAWALA MKOA WA DODOMA

Na.Sofia Remmi. Habari-Dodoma Rs Uongozi wa Bank ya PBZ umemtembelea Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya ofisini kwake jengo la Mkapa Jijini Dodoma,mapema Februari 19,2025. Lengo la ziara hiyo ni kusalimia na kuzungumza kuhusu fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo katika Mkoa wa Dodoma. Uongozi huo uliambatana na Meneja wa Benki ya PBZ Dodoma Bi. Mwanaharusi Ally na Afisa Mahusiano Abdul Khamis. #dodomafahariyawatanzania. #keroyakowajibuwangu.