
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema Mkoa wa Dodoma kwa kushiriana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida wamejipanga vizuri katika kuhakikisha vijana na watu mbalimbali wanapata fursa ya kupata Elimu kupitia maonyesho ya Wakulima na wafugaji (Nananane). Senyamule ameyasema hayo leo julai 31/2023 Ofisini kwake Jengo la Mkapa alipozungumza na waandishi wa Habari kuhusu Sherehe na Maonyesho hayo yanayotarajiwa kuanza Agosti mosi na kilele chake ni Agosti 8 mwaka huu katika viwanja vya Nane nane Nzuguni Jijini Dodoma. "Katika maonyesho hayo kutakuwa na Teknolojia mbalimbali za kuongeza tija na faida katika mnyororo wa thamani, wadau watapata fursa za kubaini Teknolojia zitakazoongeza tija katika uzalishaji. Senyamule amesema kuwa Dhamira ya maonyesho ya mwaka huu ni kuongeza hamasa ya uzalishaji wenye tija,kusambaza mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi na uharibifu wa mazingira,kutoa ajira kwa vijana na kusambaza teknolojia za kisasa kat...