"UTUNZAJI MAZINGIRA NI SUALA LA KIIMANI KWANI NI AGIZO LA MUNGU" RC SENYAMULE

Wito umetolewa kwa waumini wa Madhehebu mbalimbali, kuzingatia utunzaji wa Mazingira kwa kutumia nishati Safi kwani ni moja kati ya maagizo ya Mungu. Hayo yamesemwa wakati wa kufunga Kongamano la Maombi ya toba ya urejesho wa thamani ya Afrika 2024. Kongamano hilo kubwa lililofanyika kwa siku tatu kwenye ukumbi wa Mwangata uliopo Barabara ya Singida Jijini Dodoma, limefungwa June 28, 2024 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule na lilishirikisha wanamaombi na wachungaji kutoka nchi tano za Afika. "Mazingira ni Imani kwani Mungu ametuagiza tutunze Mazingira. Tuungane katika matumizi ya nishati Safi ili kulinda mazingira yetu yanayoweza kuathiri Dunia nzima. Kupitia Maombi haya, naona mabadiliko kwa Dodoma na Afrika kwa ujumla kwani suala hili limewakutanisha viongozi wetu wakubwa wa nchi mbalimbali" Amesema Mhe. Senyamule Akisoma risala yake mbele ya mgeni rasmi, Askofu Daniel Kitua wa Kanisa la Talitha Cuni na Mratibu wa Kongamano, Maombi hayo yameleta mafanikio c...