Posts

Showing posts from March, 2025

RAIS SAMIA ATOA MKONO WA EID KWA WENYE UHITAJI DODOMA

Image
  Mkuu Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule aki washukuru na kuwapongeza walezi wanaolea watoto kwenye vituo vya  mahitaji maalum wakati alipokwenda kutoa zawadi za mkono wa Eid zilizotolewa na  Mhe. Rais Samia kwenye vituo vya  Kijiji cha Matumaini na Rahman ‘Orphanage Center Jijini Dodoma Machi 30, 2025 Kiongozi wa Kijiji cha Matumaini Padri Vicent Boselli akizungumzia namna kituo chake kinavyolea watoto wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa zaidi ya miaka 20 sasa  wakati Mhe. Senyamule alipokwenda kutoa zawadi za mkono wa Eid zilizotolewa na  Mhe. Rais Samia kwenye vituo vya  Kijiji cha Matumaini na Rahman ‘Orphanage Center Jijini Dodoma Machi 30, 2025 Picha juu na  chini ni baadhi ya watotyo wanaolelewa kwenye kituo cha KIjiji cha Matumaini walipotembelewa na Mh. Senyamule kwa ajili ya kupewa zawadi za mkono wa Eid zilizotolewa na  Mhe. Rais Samia kwenye vituo vya  Kijiji cha Matumaini na Rahman ‘Orphanage Center Jijini Dodo...

VISIMA 7 VYA UMWAGILIAJI KULETA MAPINDUZI MAKUBWA KWENYE KILIMO DODOMA

Image
  Na. Hellen M. Minja,        Habari – DODOMA RS Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kufanya Mapinduzi makubwa kwenye Sekta ya Kilimo Mkoa wa Dodoma kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ambapo Machi 28,2025 Tume hiyo imefanya uzinduzi wa Mradi wa uchimbaji wa visima 7 vya umwagiliaji katika Kata ya Matumbulu Jijini humu. Akizindua mradi huo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema kuwa Mapinduzi haya yanahitaji ushirikiano wa pande zote mbili ili kuleta matokeo chanja katika Kilimo. “Haya ni Mapinduzi lakini yanataka pande zote, upande huu wa Serikali Mhe. Rais anakua amemaliza kwa kujenga kisima, upande wenu ni kuhakikisha  taratibu zote za kutumia hii rasilimali, kisima hiki kilete tija inayokusudiwa na Serikali na faida kwa maisha yenu kama matamanio ya Serikali yalivyo.” Akizungumza na Wananchi hao, Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mhe. Anthony Mavunde, amesema kazi ya uchimbaji wa kisima inayofanyika hapo inakwenda kuongeza wigo mpana kwa ...

LISHE BORA : KICHOCHEO CHA MAENDELEO ENDELEVU KATIKA JAMII

Image
  Na Sofia Remmi. Habari Dodoma RS  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule, ameiasa jamii kuzingatia suala la lishe Bora kutokana na umuhimu wake.  Mhe Senyamule ametoa kauli hiyo wakati akiendesha kikao cha tathmini ya utekelezaji wa Mkataba wa  Lishe  kwa Kipindi cha Julai- Disemba 2024. Kikao hicho kimefanyika  Machi 28,2025 katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma (Manispaa ya Zamani). "Lishe ni jambo muhimu, tukifanikiwa watu wakaelewa vizuri kuhusu lishe,wale vizuri,watu wakila vizuri,mengine yote yatakaa vizuri" Amesisitiza Mhe. Senyamule. Awali akifungua kikao hicho, Mhe.Senyamule amesema  ni dhahiri kuwa, lishe bora katika jamii ni kichocheo cha maendeleo endelevu katika nyanja zote na hasa ya viwanda, afya, kilimo, elimu, biashara, uchumi. “Athari za lishe duni au utapiamlo zitakapodhibitiwa au kutokomezwa ndipo malengo ya maendeleo katika nyanja hizi yataweza kufikiwa kwa ufanisi. Tafiti ya kidemografia ya mwaka 2022...

VIJANA WAASWA KUTOJIINGIZA KWENYE MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA

Image
  Na Sofia Remmi. Habari-Dodoma Rs Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mheshimiwa Rosemary Senyamule amewataka Vijana kuacha kujaribu kila kitu,kwani kwa kufanya hivyo,baadhi yao wamejikuta wakijiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya ambayo matokeo yake ni kumomonyoka kwa maadili na kupotea  kwa nguvu kazi ya Taifa. Mhe. Senyamule ameyasema hayo Machi 28,2025  wakati wa Kongamano la Vijana la Kupinga Matumizi ya Dawa za kulevya  lililoandaliwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kushirikiana na Tasisi isiyo ya kiserikali ya Taifa Forum. "Sumu haionjwi,Wazee sio wepesi kujaribu kila kitu.Lakini Vijana mmekuwa wepesi kujaribu kila kitu, katika kujaribu huko, mnajikuta mmeingia kwenye kutumia Dawa za kulevya,kitu ambacho kinaharibu maisha yenu,kinasababisha mmonyoko wa maadili,lakini pia kinapunguza nguvu kazi ya Taifa.Acheni kujaribu kila kitu, ukiambiwa kitu hiki hakifai,acha,usijaribu kukifanya".Amesema Mhe. Senyamule Mhe. Senyamule ameongeza kuwa nguv...

EACOP WAASWA KUACHA ALAMA KWA WANANCHI WANAOPITIWA NA MRADI

Image
     Na. Hellen M. Minja, Habari – DODOMA RS Uongozi unaosimamia Mradi wa ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kipande cha Dodoma, umesisitizwa kuzingatia sheria ya kurudisha kwa jamii kupitia Mradi huo unaotekelezwa katika kijiji cha Seria, Kondoa na Wilaya ya Chemba kwani wananchi wanatakiwa kuona alama iliyoachwa na mradi unaopita kwenye maeneo yao. Msisitizo huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule alipokua akizungumza na uongozi huo pindi ulipotembelea ofisini kwake Jengo la Mkapa Jijini Dodoma Machi 28, 2025 kwa lengo la kuwasilisha maendeleo ya utekelezaji wa Mradi huo. “Mnaweza kuweka kisima na zile njia za umwagiliaji, utakuta hata sehemu ya heka 100 inamwagiliwa sehemu moja, matokeo yake yatakua makubwa na kisima kitadumu muda mrefu na ndio mwelekeo wa Serikali na Wizara ya Kilimo tupate kilimo cha muda mrefu na si kutegemea mvua. Kwa sababu hiyo, pamoja na yote, nendeni mkafanye hivyo”. Aidha, Katibu Tawala Mkoa...

WAUGUZI VIONGOZI WATAKIWA KUSIMAMIA UTOAJI WA HUDUMA BORA ZA AFYA

Image
  DODOMA Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Dkt. Festo Dugange amewaelekeza Wauguzi Viongozi wa ngazi zote za afya Nchini,  kuhakikisha wanaimarisha usimamizi wa utoaji wa huduma bora ili wananchi wote wapate huduma bora na kwa usawa. Dkt. Dugange ameyasema hayo Machi 27, 2025 wakati akifungua mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wauguzi Viongozi uliofanyika katika ukumbi wa  Mikutano wa PSSSF  Jijini Dodoma wenye kauli mbiu inayosema 'HUDUMA BORA, WAJIBU WANGU'. Amefafanua kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya, lakini  bila ya kuwepo kwa  huduma nzuri na bora kutoka kwa watoa huduma za afya, na hasa Wauguzi, uwekezaji huo hautakua na manufaa. “Serikali imefanya uwekezaji mkubwa  kwenye sekta ya afya ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya afya, ununuzi wa vifaa na vifaa tiba, uboreshaji wa mazingira ya kazi, hivyo mnapaswa kuwasimamia waliopo chini yenu ili wafanye kazi kwa weledi na ua...

RC SENYAMULE AWASHUKURU WANADODOMA KWA UPENDO NA USHIRIKIANO KWAKE

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akiwashukuru Wanadodoma kwa upendo na Ushirikiano wanaomuonesha wakati wa hafla ya Iftar aliyoiandaa kwa makundi maalum ya kijamii Mkoani hapa Machi 27, 2025 Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya akijumuika na viongozi wengine wa Mkoa kwenye Iftar iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa kwa makundi maalum ya kijamii Machi 27, 2025 katika viwanja vya makazi yake Kilimani, Jijini hapa. Kaimu Kadhi wa Mkoa wa Dodoma Sheikh Nurdin Ramadhan, akimshukuru Mhe. Senyamule na kuwaasa Wanadodoma kumuombea dua kwa  Iftar aliyoiandaa kwa makundi maalum ya kijamii Machi 27, 2025 katika viwanja vya makazi yake Kilimani, Jijini hapa. Baadhi ya makundi maalum yanayopatikana katika Mkoa wa Dodoma yakijumuika kwenye Iftar iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa kwa makundi maalum ya kijamii Machi 27, 2025 katika viwanja vya makazi yake Kilimani, Jijini hapa. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akiwa kwenye picha za pamoja na makundi mbalimbali y...