Posts

Showing posts from April, 2025

TANROADS WATAKIWA KUTAFUTA NJIA MBADALA KWA WANANCHI WAKATI WA UJENZI WA DARAJA LA MORENA

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule (katikati), akitoa maelekezo kwa Meneja wa TANROADS Mkoa kutafuta njia mbadala kwa wakazi wa Morena wanaohitaji huduma upande wa pili wa daraja kipindi hiki cha ujenzi wakati alipotembelea mradi huo Aprili 29, 2025 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri amesema upanuzi wa daraja la Morena utamaliza changamoto ya mafuriko kwenye makazi ya watu kipindi cha mvua kubwa, changamoto za kiafya na magonjwa ya mlipuko wakati wa ziara fupi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kukagua mradi huo Aprili 28, 2025.  Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dodoma Mhandisi Zuhura Amani, amewaahidi wananchi kuwa pamoja na kuzingatia ubora, wataendelea kumhimiza Mkandarasi kukamilisha kazi hiyo mapema ili wananchi waone matunda yake  wakati wa ziara fupi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kukagua mradi huo Aprili 28, 2025. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule alipofanya ziara fupi ya kutembelea mradi wa upanuzi wa daraja la Morena litakalotatua kadhia ya ku...

DODOMA YAMALIZA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2025 NA KUUKABIDHI IRINGA

Image
  Na. Hellen M. Minja        Habari – DODOMA RS Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, leo Aprili 28, 2025 amekabidhi Mwenge wa Uhuru 2025 rasmi kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba baada ya kukimbizwa kwa KM 1333 kwenye Wilaya zote saba (7) na Halmashauri nane (8) za Mkoa huu kuanzia Aprili 20 hadi 27 ulipokamilisha Mbio zake. Akizungumza na hadhara iliyojitokeza katika makabidhiano hayo yaliyofanyika kwenye Kijiji cha Makatapora Wilaya ya Iringa, Mhe. Senyamule amesema miradi yote iliyochaguliwa imepitiwa na Mwenge huo. “Katika Mkoa wetu, Mwenge wa Uhuru umeweza kutembelea miradi 56 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 61.1 Nami nakiri kwa kusema, katika Mkoa wa Dodoma miradi yote imepitiwa, kukaguliwa, kuwekewa mawe ya msingi, kutembelewa na tumepata ‘clean sheet’.” Mhe. Senyamule ameongeza kuwa, wakati wa mbio hizo Mkoani hapa, wameweza kufanya mazoezi ya kupima Virusi vya Ukimwi, kuchangia damu na magonjwa mengine na yote yamedhihirisha k...

YALIYOJIRI;MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2025 HALMASHAURI YA WILAYA YA MPWAPWA

Image
  Na Francisca Mselemu        Habari – Mpwapwa DC Tarehe 27 Aprili 2025, Mwenge wa Uhuru ulipokelewa kwa shangwe na ari kubwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa na kukimbizwa umbali wa kilometa 234 .  Katika mbio hizo, miradi  8 yenye thamani ya jumla ya shilingi 1,118,248,505.34,ikionesha maendeleo makubwa yanayofanyika katika sekta mbalimbali za maendeleo ya jamii. Moja ya miradi muhimu ni ujenzi wa karakana ya vifaa vya kilimo katika Kijiji cha Ngh’ambi,ulizinduliwa,  gharama za mradi huu ni shilingi 55,790,000. Hii ni juhudi za kuimarisha sekta ya kilimo na kuongeza tija kwa wakulima wa eneo hilo. Pia, zahanati ya  Kijiji cha Ngh’ambi iliwekewa jiwe la msingi kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya afya,  gharama za mradi huu ni shilingi 65,000,000, ikiwa ni hatua muhimu ya kuboresha huduma za afya kwa Wananchi wa Kijiji hicho. Katika sekta ya miundombinu, ujenzi wa daraja jipya la Chifu Mkunda mjini Mpwapwa umefanyika, gharam...

YALIYOJIRI; MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2025 HALMASHAURI YA WILAYA YA WILAYA YA BAHI

Image
  Katika siku ya kihistoria ya tarehe 25 Aprili 2025, Mwenge wa Uhuru ulikimbizwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bahi  umbali wa Kilometa 164 ambapo ulipitia miradi 6, yenye thamani ya shillingi 1,517,657,312.63 .Miradi hiyo ni kama ifuatavyo; Ujenzi wa Daraja la Mgondo, Barabara ya Zamahero - Asanje - Kogogo,ulizinduliwa rasmi na unagharimu shilingi 153,559,166.3. Daraja hili litasaidia kuboresha usafiri na ushirikiano kati ya vijiji vinavyopitiwa na barabara hii. Ujenzi wa Miundombinu ya Afya na Usafi wa Mazingira katika Zahanati ya Mayamaya,Mwenge ulitembelea mradi huu wenye thamani ya shilingi 52,000,000. Ujenzi huu ni muhimu katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi wa eneo hilo. Kikundi cha Vijana Maua Zanka .Mradi huu wenye thamani ya shilingi 20,000,000 ulitembelewa na Mwenge. Utekelezaji wa mradi huu ni sehemu ya juhudi za  Serikali  kuwajengea uwezo vijana katika shughuli za kiuchumi. Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Kisima cha Nd...

KILELE CHA MAADHIMISHO YA MUUNGANO WA TANZANIA: MSISITIZO WATOLEWA JUU YA ULINZI WA MUUNGANO

Image
  Na. Hellen M. Minja,        Habari - DODOMA RS  Ikiwa ni kilele cha Maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, 2025 ambayo yamekwenda sanjari na hitimisho la ziara ya siku nne (4) ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Stephen Wasira katika Mkoa wa Dodoma, ametembelea miradi kadhaa ya maendeleo katika Halmashauri za Chemba, Kondoa na Kondoa Mji sambamba na kuongea na wananchi kwenye Halmashauri hizo. Katika kilele cha Maadhimisho hayo, Ndugu Wasira ameendelea kusisitiza juu ya kutunza Muungano wetu ambao waasisi wake Hayati Mwl. Nyerere, Rais wa kwanza wa Tanganyika na Hayati Abeid Karume, Rais wa kwanza wa Zanzibar waliupigania na kuzaliwa nchi ya Tanzania kwa ajili ya kutunza Amani na maendeleo ya vizazi vyote. "Kuwa na nchi mbili kama hazielewani, matatizo ya kiusalama ni makubwa sana, moja ya sababu zilizofanya tukaungana ni kuweka nguvu ya pamoja kwa ajili ya kuweka amani ambayo ndio msingi wa Maendeleo yote mnayoya...

YALIYOJIRI;MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2025 HALMASHAURI YA WILAYA YA KONDOA

Image
  Na Francisca Mselemu       Habari - Kondoa DC Tarehe 23 Aprili 2025,Mwenge wa Uhuru ulikimbizwa katika halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kwa umbali wa kilometa 154.9.  Katika mbio hizo, mwenge ulipitia miradi 7 yenye manufaa kwa jamii, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha maendeleo na kuonyesha juhudi za Serikali  ya awamu ya sita katika kuboresha maisha ya wananchi.Miradi hiyo ni ; Mradi wa maji safi na usafi wa mazingira katika Zahanati ya Itundwi.Ulizinduliwa, Gharama shilingi  50,000,000, mradi huu unalenga kuboresha upatikanaji wa maji safi ili kuimarisha usafi wa mazingira ya eneo hilo . Mradi wa matumizi ya Nishati Safi. Ulikaguliwa, gharama, shilingi  5,000,000,unahusisha matumizi ya nishati mbadala, kusaidia kupunguza utegemezi wa nishati zisizokuwa rafiki kwa mazingira na afya za watumiaji. Mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Kijiji cha Filimo.Uliwekewa jiwe la msingi, gharama, shilingi 32,549,053.9 utasaidia katika usimamizi wa shughuli za kijiji na ...

VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI WATAKIWA KUZINGATIA UTAWALA BORA NA DEMOKRASIA

Image
  Na; Happiness E. Chindiye       Habari - Dodoma Rs  Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania Bara Ndugu, Stephen Wasira ametoa wito kwa viongozi wa vyama vya Siasa Nchini kuheshimu Misingi ya Utawala bora na Demokrasia ikiwa ni pamoja na kutoingilia mienendo ya Mashauri yaliyo kwenye vyombo vya dola ili kuruhusu haki kutendeka kwa uhuru. Wasira ametoa wito huo jijini Dodoma Leo Aprili 25,2025 wakati akizungumza na wanachama na wananchi katika mkutano wa hadhara ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi inayotekelezwa na Serikali kupitia Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020/25.   “Viongozi wa siasa heshimuni utawala na demokrasia ili kusaidia vyombo vya dola kufanya maamzi kwa uhuru”. Wasira Naye ,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule ameeleza kuhusu utatuzi wa changamoto zinazowakabili wananchi ikiwamo kero ya Maji katika jiji la Dodoma. Katika ziara hii Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Stephen Wasira Jijini Dodoma ametembelea mi...