Posts

Showing posts from June, 2025

SERIKALI IMEJIZATITI KULETA MAENDELEO KWA KUIMARISHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA

Image
       Na. Happiness E. Chindiye      Habari - Dodoma RS  Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Uongozi madhubuti wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejizatiti kuleta maendeleo edelevu katika taifa la Tsnzania, ikiwemo kuboresha na kuimarisha mazingira ya uwekezaji na biashara Nchini.  Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule wakati akifunga maadhimisho ya kitaifa ya udhibiti wa bidhaa bandia Duniani yaliyofanyika katika ukumbi  wa Mabele Jijini Dodoma. Tarehe 25.06.2025. “Kupitia uwezeshaji wa Serikali kwa wananchi waliojiunga kwenye vikundi na kupatiwa mikopo katika ngazi mbalimbali, zikiwemo Mikoa na Wilaya, vikundi vya uzalishaji vinaendelea kupata nguvu ya kutengeneza bidhaa zilizo halisi na bora, baada ya kupatiwa mafunzo ya ujasiriamali kutoka SIDO, TBS, BRELA na FCC. “Serikali kuendelea kuiamini na kuiwezesha Tume ya Ushindani kusimamia usalama wa soko, utimamu ...

“TANZANIA SIO SALAMA KWA WAUZAJI, WASAFIRISHA, WALIMAJI NA WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA” MHE. MAJALIWA

Image
  Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akihutubia hadhira iliyojitokeza kwenye kilele cha Maadhimisho ya siku ya kupiga vita matumizi na biashara ya dawa za kulevya Duniani kwa niaba ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Juni 26, 2025 katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma. Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya (DCEA), Aretas Lymo akitoa takwimu za ukamataji wa dawa za kulevya wakati wa  kilele cha Maadhimisho ya siku ya kupiga vita matumizi na biashara ya Dawa za Kulevya Duniani kilichafanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma Juni 26, 2025. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, akizungumzia jitihada za Mkoa wake kupambana na Dawa za Kulevya  wakati wa  kilele cha Maadhimisho ya siku ya kupiga vita matumizi na biashara ya Dawa za Kulevya Duniani kilichafanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma Juni 26, 2025. Waziri...

RC SENYAMULE AZINDUA JENGO LA KUPUMZIKIA WAGONJWA HOSPITALI YA MKOA

Image
Na: Sofia Remmi Habari:DodomaRs Mkuu wa Mkoa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amezindua Jengo la kupumzikia ndugu wa wagonjwa katika hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma,Leo tarehe 25 Juni 2025 Katika Viwanja vya Hospital hiyo Jijini Dodoma. Akizungumza wakati wa Hotuba yake Mhe. Senyamule amewataka   wadau wengine wa Serikali na ambao sio wa Serikali kuendelea kuunga Mkono Jitihada mbalimbali za Kiserikali kama alivyofanya  Waziri wa Madini na Mbunge wa Jiji la Dodoma Mhe. Mbunge Anthony Mavunde kwa kufanya Ukarabati  katika jengo la kupumzikia ndugu wa Wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma. "Nitoe wito kwa Wadau wengine waendelee kujitokeza kuunga Mkono  jitihada zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Dkt.Samia Suluhu Hassan kama alivyofanya Mbunge". Kadhalika, Mhe. Senyamule, amewataka watumishi wa Hospitali hiyo kuendelea kuchapa kazi zaidi ili huduma ziendelee kuwa bora. Kwa upande wake Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa y...

SHUGHULI ZA KIBINADAMU ZATAJWA KUWA TISHIO KWA CHANZO CHA MAJI BONDE LA MAKUTUPORA JIJINI DODOMA

Image
  Na. Hellen M. Minja   Habari – DODOMA RS Uvamizi wa vyanzo vya maji kwa shughuli za kibinadamu unatajwa kuwa changamoto inayoendelea kuvikabili vyanzo vya Maji hususan kile cha Bonde la Makutupora (Kidakio cha Kinyasungwe).  Hayo yamebainishwa wakati wa kikao cha jukwaa la Wadau wa maji sekta Mtambuka Kidakio cha Kinyasungwe Jijini Dodoma. Kikao hicho kilichoongozwa na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya, kimefanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya ‘Midland View Inn’ Kisasa Jijini hapa, kimelenga kujadili mambo kadhaa yanayokikabili Kidakio hicho ambacho ni chanzo muhimu cha maji kwa Jiji la Dodoma. “Kuna uvamizi wa vyanzo vya maji vinavyotegemewa na Jiji la Dodoma kama vile maeneo tengefu ya hifadhi ya maji chini ya ardhi. Uvamizi huu upo maeneo mengi mno, kuna wengine wanakwenda kulima, kukata miti na shughuli nyingine. Hii changamoto ishughulikiwe, eneo lile litunzwe kwani faida yake tunayo sisi Wanadodoma”. Bw. Mmuya Kadhalika, Mkurugenzi wa Bodi ya Maji B...

VODACOM TANZANIA KUPANDISHA HADHI MINARA YAO KUIMARISHA MAWASILIANO DODOMA

Image
  Picha tofauti za   Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akiwa kwenye mazungumzo na  Mkuu wa Kanda Vodacom Bi. Chiha Nchimbi pamoja na  Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano ya Nje Vodacom Bi. Zuwena Farah walipomtembelea ofisini kwake leo Juni 25, 2025.   Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule (katikati) katika picha ya pamoja na Mkuu wa Kanda Vodacom Bi. Chiha Nchimbi (Kulia) na  Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano ya Nje Vodacom Bi. Zuwena Farah walipomtembelea ofisini kwake leo Juni 25, 2025 kwa lengo la kuji tambulisha  Na. Hellen M. Minja        Habari – DODOMA RS Kampuni ya mawasiliano ya simu Vodacom ipo kwenye Mpango wa kuifanyia ukarabati minara yake zaidi ya 50 iliyopo Jijini Dodoma kwa kuipandisha kutoka 3G kwenda 4G na 5G kwa lengo la kuimarisha mawasiliano kutokana na changamoto za kimawasiliano kwenye maeneo yenye minara ya 3G. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kanda Vodacom Bi. Chiha Nchimbi ali...

SERIKALI IMEJIPANGA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA : WAZIRI GWAJIMA

Image
  Na; Happiness E. Chindiye  Habari - Dodoma RS  Serikali imejipanga vema kupambana na tatizo la dawa za kulevya kwa kuanzisha chombo mahsusi kijulikanacho kama Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), ambacho pamoja na majukumu mengine ina jukumu la kupunguza madhara yatokanayo na matumizi ya dawa za kulevya, kuratibu na kusimamia masuala ya tiba na huduma za utengamao kwa waraibu wa dawa za kulevya Nchini ikiwemo nyumba za upataji nafuu.  Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mandeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Doroth Gwajima wakati la Kongamano la Vijana lililo andaliwa mahususi kwa ajili ya elimu juu ya tatizo la dawa za kulevya lililofanyika ukumbi wa Mabele Jijini Dodoma. “Mamlaka yetu ina jukumu la kutoa elimu sahihi kwa Umma juu ya athari za biashara na matumizi ya dawa za kulevya, kuhamasisha jamii kushiriki katika mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya.  “Kwa hiyo tukio letu la leo linashabihiana kabisa na mal...