DUWASA YAJIPAMBANUA UHAKIKA WA MAJI DODOMA
Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira Mkoa wa Dodoma (DUWASA) inaendelea kufanikisha lengo la upatikanaji wa maji kwa asilimia 100 kwa Mkoa wa Dodoma kufuatia juhudi za Serikali ya awamu ya Sita. Hayo yamebainishwa wakati wa mfululizo wa vipindi maalumu vya kutangaza mafanikio ya Serikali kwa Taasisi za Umma vilivyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambapo leo kimeangazia sekta ya maji. Akiwasilisha hotuba yake mbele ya wanahabari wakati wa utangulizi wa kipindi hicho, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameelezea miradi mbalimbali ya maji inayoendelea katika Mkoa na utekelezaji wake ndani ya kipindi hiki cha miaka miwili ya Serikali ya awamu ya sita. “Tunafahamu maji ni kila kitu katika maisha ya mwanadamu, maji ni Uhai. Katika Mkoa wa Dodoma, kumekuwa na Uendelezaji wa vyanzo vya maji (uchimbaji wa visima na ujenzi wa mabwawa) kwa kutumia vyanzo vikuu kama vile Uchimbaji wa visima virefu 34, Ujenzi wa Mabwawa 2 ya maji, miradi 10 ya maji inayotumi...