DODOMA YAJIPANGA KUINUA ELIMU
Idara ya Elimu Mkoa wa Dodoma imefikia maazimio kadhaa yenye lengo la kuinua sekta ya Elimu kwenye Mkoa wakati wa kikao kazi kilichowashirikisha wadau mbalimbali wa Elimu chini ya Mwenyekiti wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule na Katibu Tawala Mkoa Bw. Ally Gugu kwenye ukumbi wa TAG - Mipango Miongoni mwa maazimio hayo ni pamoja na kuanzishwa kwa mfuko wa Elimu kwenye kila Halmashauri ili kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu, utoaji wa chakula shuleni, kuthibiti utoro, hili, kila shule kuhakikisha kila mwanafunzi anamudu mada inayofundishwa, kila mwanafunzi anayemaliza Elimu ya Msingi anaanza masomo ya kujiandaa na kidato cha kwanza wiki mbili baada ya kufanya Mitihani. Mhe. Senyamule amesema matarajio ya Serikali ya awamu ya sita ni kuona maendeleo makubwa kwenye sekta ya Elimu kutokana na uwekezajj Mkubwa uliofanyika ...