CHAMWINO DC YATAKIWA KUJITAFAKARI

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kukamilisha ujenzi wa uzio wa ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kabla ya tarehe 30/3 / mwaka huu. Maagizo hayo yametolewa Leo Februari 21,2024 baada ya kuonekana kudorola Kwa mradi huo Kwa zaidi ya miezi 8 tangu ulipotakiwa kukamilika mwezi julai 2023. "picha ya Chamwino Kwa Sasa siyo nzuri, Mkoa una Halmashauri nane na katika Halmashauri hii kila miradi inayokuja lazima zijitokeze changamoto, tunapokea malalamiko yenu mengi hasa suala la malipo Kwa wakandarasi wanaojenga miradi yenu, Mhe.Rais anatoa fedha zote ila nyie mnachelewesha kuwalipa na hiyo ndio sababu inachangia mradi kutokukamilika kwa wakati. nitoe maagizo tarehe 30/03/2024 mradi uwe umekamilika kwa ubora wake na ukamilike kwa fedha ambazo zilitolewa na ikiwezekana fedha zibaki na zifanye kazi nyingine". Ameelekeza Mhe.Senyamule Aidha Mhe. Senyamule amemsimamisha kazi mtendaji wa kata ya...