UKILETWA DODOMA UMELETWA KUJENGA MAKAO MAKUU YA NCHI
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amemuapisha Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe. Gerald R. Mongella pamoja na kuwapokea Wakuu wa Wilaya wapya wawili waliohamishiwa Mkoa wa Dodoma kwenye hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa jengo la Mkapa zilipo Ofisi za Mkuu wa Mkoa. Mhe. Senyamule amewaasa Wakuu hao wa Wilaya kuheshimu nafasi waliyopewa na Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwani wameaminika kuitumikia nafasi hiyo. “Nafasi ya Ukuu wa Wilaya ina madaraka na dhamana kubwa sana, ukiyatumia kwa tija yanaleta manufaa ila ukiyatumia vibaya utakwenda kupata matokeo mabaya” Aidha Mhe. Senyamule amesema kuwa Dodoma ni Makao Makuu ya nchi na nafasi waliyopewa wakuu hao ni kuja kuijenga Makao Makuu. “Kuja Dodoma ni bahati kwakuwa mnakuwa sehemu ya kujenga Makao Makuu ya nchi. Yeyote aliyekuja hapa, ajue amepata nafasi ya kujenga Makao Makuu kwani viongozi wetu wakuu wana matarajio makubwa na sisi. Mkoa umejipanga kuifanya Makao Makuu kama yalivyo matarajio ya viongozi wetu” Mhe....