Posts

Showing posts from December, 2024

RC SENYAMULE AKABIDHIWA CHETI CHA SHUKRANI NA SHIVYAWATA DODOMA

Image
Na. Hellen M. Minja,        Habari – DODOMA RS Uongozi wa Muungano wa Vyama vya Watu Wenye Ulemavu SHIVYAWATA leo Disemba 31, 2024 wamefika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma iliyopo katika jengo la Mkapa Jijini Dodoma kwa lengo la kumshukuru Mkuu wa Mkoa Mhe. Rosemary Senyamule kwa kufanikisha hafla ya chakula cha pamoja wakati wa maadhimisho ya siku ya walemavu Duniani yaliyofanyika Disemba 6, 2024. Shukrani hizo zimekwenda sanjari na kumkabidhi cheti cha shukrani kwa kutambua mchango wake wa hali na mali katika kufanikisha Kongamano la siku mbili kuelekea maadhimisho hayo lililofanyika Disemba 5 na 6 katika Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Waliofika ofisini hapo kwa niaba ya uongozi ni Bw. Jastus Ngwantalima na Bw. Enock Mbana.   Kauli mbiu iliyoongoza Maadhimisho ya mwaka huu ilikua “Kukuza Uongozi wa Watu Wenye Ulemavu kwa Ajili ya Mustakabali Jumuishi na Endelevu" #dodomafahariyawatanzania                    ...

RC SENYAMULE ASHIRIKI CHAKULA CHA MCHANA NA WENYE MAHITAJI.

Image
Na. Sizah Kangalawe Habari- Dodoma Rs  Ikiwa ni kipindi Cha maadhimisho ya sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameshiriki hafla ya Chakula cha pamoja na watoto yatima na waishio katika mazingira  magumu wapatao 300 pamoja na wajane 100 wanaohudumiwa na kufadhiliwa na shirika la Tumaini foundation Jijini Hapa.  Hafla hiyo imefanyika Disemba 26 katika ukumbi wa Lavana uliopo Ihumwa Jijini Dodoma.  Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mhe. Senyamule amempongeza Mkurugenzi wa Shirika hilo Ndg. Tumaini Kivuyo kwa Moyo wa huruma wa kuwasaidia na kuyahudumia Makundi maalum kwani shirika hilo linalenga kuwahudumia watoto yatima, watoto wanaofanya kazi mitaani kabla ya umri wao wa kujitegemea pamoja wajane ambao hupatiwa huduma za Elimu, Ujasiriamali, Matibabu pamoja na kuwawezesha kiuchumi. Aidha Mhe. Senyamule ametumia wasaa huo kukemea vikali tukio la mauaji ya mtoto wa miaka 6 lililotokea Disemba 25, 2024 Kata ya Ilazo Jijini Dodo...

RC SENYAMULE NA STAMICO WASHIRIKI CHAKULA CHA PAMOJA SAMARIA - HOMBOLO

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, akizungumza na wazee wa kijiji cha Samiria aliposhiriki chakula cha pamoja na kundi hilo la wazee wenye ugonjwa wa ukoma wanaoishi katika Kata ya Hombolo Bwawani, Jijini Dodoma Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akimlisha keki Mmoja wa wazee wa Kijiji cha Samaria alipofika kushiriki chakula cha pamoja na kuwashika mkono kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka Baadhi ya wana kikundi cha Wanawake na Samia cha Mkoa wa Dodoma wakigawa chakula kwa watoto wa kijiji cha Samaria wakati wa hafla ya kuwashika mkono wazee wa kijiji hicho kwa kutoa misaada na kushiriki chakula cha pamoja Baadhi ya Wazee wa kijiji cha Samaria kilichopo Hombolo Jijini Dodoma wakipiga makofi wakati wa hafla ya chakula cha pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Senyamule na Mkurugenzi Mtendaji  wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Disemba 23, 2024 Baadhi ya Wazee wa Samaria (picha juu na chini) wakipokea misaada iliyopelekwa kijijini hapo n...

"WANANCHI TOENI TAARIFA JUU YA VITENDO VYA UKATILI" -RC SENYAMULE.

Image
Na Sofia Remmi. Habari-Dodoma Rs  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule ameyasema hayo leo tarehe 23 Disemba 2024 katika kikao cha Mpango kazi wa Taifa wa Kutokomeza ukatili dhidi wanawake na watoto (MTAKUWWA). Akizungumza na wajumbe wa kamati iyo Rc Senyamule amesema wananchi wanatakiwa kutoa taarifa juu ya vitendo vya ukatili vinavtofanyika mahali popote walipo. Ameongeza kuwa, kamati ya Ulinzi wa wanawake na watoto Mkoa wa Dodoma, imeanzisha mpango kazi huo ili kupunguza na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake, watoto na wanaume. “Ukatili husababisha athari nyingi ikiwemo mimba za utotoni, ulemavu na kuambukizwa VVU na UKIMWI. Serikali ya awamu ya sita imejipanga thabiti kupambana na ukatili wa aina yoyote unaotokea Katika Jamii. “Pia, vitendo vya ukatili husababisha kutoshiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi na kuigharimu Serikali fedha nyingi katika shughulikia vitendo vya ukatili” Mhe. Senyamule. Pamoja na juhudi mbalimbali za kutoa elimi kwa Jamii dhidi ya vi...

RC SENYAMULE AZIAGIZA HALMASHAURI ZA DODOMA KUUNDA KAMATI ZA ULINZI NGAZI YA KATA

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule akizungumza wakati wa kikao cha kujadili na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto ya watoto wanaoishi na kufanya kazi za mitaani kilichofanyika  kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji Mtumba Dodoma. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule (katikati) , Meya wa Jiji la Dodoma Prof. Davis Mwamfupe (kushoto) na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Injinia Happiness Mgalula wakiwa katika kikao cha kujadili na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto ya watoto wanaoishi na kufanya kazi za mitaani kilichofanyika  kwenye ukumbi wa Hlmashauri ya Jiji  ya Jiji la Dodoma uliopo Mtumba. Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dodoma Bi. Josephine Mwaipopo akiainisha sababu zinazochangia uwepo wa watoto wa mtaani na ombaomba katika Mkoa wa Dodoma wakati wa kikao cha kujadili namna ya kukabiliana na changamoto ya watoto wa mtaani Jijini humu.   Baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Dodoma wakisikiliza kwa maki...

NSSF KUFANYA UWEKEZAJI WA ZAIDI YA BILIONI 148 DODOMA

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akizungumza na wananchi pamoja na watumishi wa NSSF wakati wa zoezi la upandaji miti kwenye eneo la mradi wa uwekezaji unaotarajiwa kuimarisha uchumi wa Mkoa wa Dodoma pindi utakapokamilika. Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Bw. Masha Mshomba, akizungumzia uwekezaji wa NSSF ndani ya makao makuu ya nchi Dodoma kuwa ni jukumu la kipekee waliloamua kulifanya na litakwenda kuleta tija katika ongezeko la mapato ya mfuko huo. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akiotesha mti katika eneo linalotarajiwa kuanza mradi wa jengo la ghorofa 16 chini ya NSSF lililopo Njedengwa Jijini Dodoma Disemba 20, 2024. Baadhi ya watumishi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF, wakiotesha miti wakati wa zoezi hilo lililofanyika kwenye eneo linalotarajiwa kuanza mradi mkubwa wa uwekezaji Njedengwa, Jijini Dodoma. Baadhi ya watumishi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani) baada ya kukamilika kwa zoezi la uoteshaji miti kwen...

DODOMA NA MIKAKATI MADHUBUTI YA KUKUZA UCHUMI.

Image
Mkuu wa MKoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule akizungumzia namna Mkoa wa Dodoma unavyokua kwa kasi kiuchumi katika kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa wa Dodoma kilichofanyika jana katika ukumbi wa Hoteli ya Vizano Jijini Dodoma. Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia akitaja vitengeneza fursa ambavyo vinapaswa kutumika ipasavyo ili kukuza uchumi kuwa ni Malikale wakati wa kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa wa Dodoma kilichofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Vizano Jijini Dodoma. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule (katikati) akimkabidhi cheti Balozi wa Mkoa wa Dodoma nchini China Bw. Japhet Konzo mara baada ya kufunga kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa wa Dodoma  Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa wa Dodoma wakifuatilia kwa makini mawasilisho mbalimbali wakati kikao hicho kikiendelea hapo jana katika ukumbi wa Hoteli ya Vizano Jijini Dodoma Na. Sizah Kangalawe Habari- Dodoma Rs  Uchumi wa  Wananchi wa Mkoa wa Dodoma unaendelea kukua siku hadi  siku ...

MTI WANGU BIRTHDAY YANGU DESEMBA, YAPANDA MITI 400 JK SQURE

Image
 Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar Mmuya akizungumza wakati wa hafla ya kupanda miti 'Team December' kuendeleza kampeni ya 'mti wangu birthday yangu' katika viwanja vya JK Square UDOM Jijini Dodoma Kampeni iliyozinduliwa rasmi Oktoba 18, 2024 katika Chuo hicho. Kamishna Msaidizi Mwandamizi Jeshi la Uhifadhi, Mkuu wa Ofisi ya Mahusiano TANAPA Dodoma Dkt. Noelia A. Myonga akielezea namna alivyofarijika na zoezi la kukijanisha Dodoma katika eneo la JK Square kwani linakumbusha uumbaji wa Mungu   Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Winiesta Saria akizungumza na hadhira iliyoshiriki kampeni ya mti wangu birthday yangu katika eneo la JK Squre ndani ya Chuo Kikuu cha Dodoma na kusema kuwa  kupanda miti ni ajenda ya Chuo hicho. Mmoja kati ya wazaliwa wa mwezi Disemba akipanda mti wakati wa Kampeni ya mti wangu birthday yangu ambayo hufanyika kila tarehe 18 ya mwezi ambapo mwezi huu iliendelea kufanyika katika eneo la JK Square (UDOM) ambapo miti 400 ilipandwa. Baadhi ya waz...

RC SENYAMULE ATAKA HATUA KALI ZICHUKULIWE DHIDI YA WANAOHUJUMU MIUNDOMBINU YA SERIKALI

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Mwenyekiti wa kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa Mhe. Rosemary Senyamule akitoa maagizo wakati wa kufunga kikao hicho hapo jana Disemba 18, 2024 ambapo alitaka Wakuu wa Wilaya kuja na Mkakati wa kuzuia wizi wa miundombinu ya Serikali. Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya akiwakumbusha wajumbe wa kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Dodoma majukumu ya kikao hicho kabla ya kuanza kikao hapo jana katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Jengo la Mkapa Jijini Dodoma Wakuu wa Wilaya za Kondoa na Mpwapwa (wa kwanza na pili kushoto) wakiwa na Makatibu Tawala wa Wilaya za Bahi na Dodoma Mjini ambao wote ni wajumbe wa kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wakifuatilia mawasilisho mbalimbali wakati wa kikao hicho. Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wakifuatilia maagizo ya Mwenyekiti wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa kikao cha kwanza kwa mwaka 2024 / 2025 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Jijini Dodoma Na. Hellen M. Minja...

SERIKALI YAKABIDHIWA KITUO CHA AFYA ILAZO.

Image
Na Sofia Remmi  Habari-Dodoma Rs. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule ameshiriki hafla ya Makabidhiano ya  Kituo cha afya  Ilazo  kilichojengwa Kwa ufadhili wa shirika la 'Korea International Cooperation Agency' ( KOICA) kwa kushirikiana na ' The United Nations Children's Fund ' ( UNICEF ).  Mashirika hayo yameikabidhi Serikali ya Mkoa kituo tayari kwa matumizi ya kuwahudumia Wananchi wa kata ya  Ilazo na maeneo jirani.  Akizungumza katika hafla hiyo Mhe. Senyamule amesema majengo hayo ya huduma za afya yamejengwa na kufadhiliwa na Shirika la la Korea KOICA Kupitia UNICEF. “Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ana lengo la kupunguza vifo vya kina mama wajawazito wakati wa kujifungua na watoto wachanga kwa kuleta huduma bora kwa wananchi wake kila kijiji na kila  mtaa. “Uboreshaji wa huduma za afya ya uzazi na mtoto imewezeshwa kwa kiasi kikubwa kwa kujenga vituo vya kutolea hiduma za afya, ununuzi wa dawa...