RC SENYAMULE NA MIKAKATI YA KUKUZA UCHUMI WA WANANCHI DODOMA

Na. Hellen M. Minja, Habari – DODOMA RS Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amekutana na Menejimenti ya Ofisi yake Februari 26, 2025, katika kikao kazi cha kujadili utendaji kazi pamoja na kupanga mikakati ya kuwezesha Mkoa kufikia malengo yake kwa mwaka huu 2025 katika ukumbi wa Hoteli ya Residence, Mipango Jijini Dodoma. Kikao hicho kiliambatana na ajenda kadhaa ikiwemo uwasilishaji wa taarifa za utekelezaji wa bajeti kuanzia mwezi Juni – Desemba, 2024, mkakati wa ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa Mkoa wa Dodoma. Aidha, Mhe. Senyamule ameitaka menejimenti hiyo kuwa na mikakati ya kukuza uchumi wa Mkoa kwani kipaumbele cha Mkoa mwaka huu ni kupandisha uchumi wa wananchi wake ili waweze kuondokana na umasikini. #dodomafahariyawatanzania #keroyakowajibuwangu #mtiwangubirthdayyangu