WATUMISHI WA OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA MAZOEZINI

Na. Sizah Kangalawe Habari- Dodoma Rs. Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma, Leo Ijumaa Januari 31, 2025 wamefanya mazoezi ya viungo vya mwili Ili kuimarisha Afya zao. Mazoezi hayo yalifanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Amani Jijini Dodoma, ikiwa ni muendelezo wa utaratibu waliojiwekea wa kufanya mazoezi kila siku ya Ijumaa ya Juma baada ya kumalizika saa za kazi na Kila jumamosi ya mwisho wa mwezi. Dhamira ya Mazoezi hayo ni kuimarisha Afya, kuepuka magonjwa yasiyoambukiza pamoja na kuimarisha mahusiano na Mshikamano baina yao.