Posts

Showing posts from November, 2024

MAFUNZO UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA YAFUNGULIWA DODOMA

Image
Na Sofia Remmi. Habari -Dodoma Rs Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe.Jaji Asina Omari ambaye pia ni Jaji wa Mahakama kuu ya Tanzania, amefungua mafunzo kwa Watendaji Ngazi ya Mkoa ya  Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga kura Leo tarehe 30 Novemba 2024. Mafunzo hayo ya siku 2  yanayoongozwa na Kaulimbiu ”Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi bora”,yanalenga  kuwajengea uwezo wa kuwafundisha Maafisa Waandikishaji Wasaidizi Ngazi ya Kata na kuhusisha namna ya ujazazi wa fomu pamoja na kutumia mfumo wa kuandikisha wapiga kura, yamefanyika kwenye ukumbi wa  Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ( Jengo la Mkapa) Wakurugenzi wa Halmashauri za Chemba,Kondoa Mji na Kondoa DC, ni miongoni mwa Washiriki wa Mafunzo hayo ambayo yatahitimishwa tarehe 01.12.2024. #kurayakosautiyako #birthdayyangumtiwangu.  

WATUMISHI RS DODOMA WASHIRIKI HAFLA YA CHAKULA CHA PAMOJA NOVEMBA

Image
Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma  leo Novemba 29,2024 wamekutana kula chakula cha pamoja  na kusherekea  kumbukizi za  siku za kuzaliwa kwa Watumishi waliozaliwa mwezi Novemba,ikiwa ni utaratibu wa kawaida uliowekwa na Uongozi kwa kila mwezi. Kama ilivyo ada,baada ya chakula na kusherekea kumbukizi za kuzaliwa,Watumishi hao walipatiwa mafunzo,ambapo  mada tatu ziliwasilishwa ambazo ni Itifaki,Lishe na Mtindo Bora wa Maisha pamoja na Umuhimu wa Mazoezi kwa Afya. #birthdayyangumtiwangu  #dodomafahariyawatanzania #keroyakowajibuwangu  

WATANZANIA 26,963,182 WAMEPIGA KURA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA : WAZIRI MCHENGERWA

Image
Na. Hellen M. Minja,        Habari – DODOMA RS Jumla ya Watanzania 26,963,182 ( Milioni ishirini na sita,laki tisa,elfu sitini na tatu,mia Moja themanini na mbili) wenye sifa za kupiga kura, wametimiza haki yao ya Kikatiba kwa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, uliofanyika Nchini kote mnamo Novemba 27, 2024. Takwimu hizo zimetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR - TAMISEMI) Mhe. Mohamed Mchengerwa (Mb) Novemba 28, 2024 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, jengo la Mkapa Jijini Dodoma alipokua akitangaza matokeo ya uchaguzi huo mbele ya Waandishi wa Habari. “Jumla ya wapiga kura 31,282,331 walijiandikisha, kati yao wanawake ni 16,450,559 na wanaume walikua 15,236,772. Wapiga kura waliohakikiwa kwa ajili ya kupiga kura walikua ni 31, 255,303. Aidha wananchi waliopiga kura siku ya tarehe 27 /11/2024 ni 26,963,182 sawa na asilimia 86.36 ya wananchi waliokua na sifa ya kupiga kura”. Mhe. Mchengerwa Aidha, a...

BENKI YA NMB YAKABIDHI KOMPYUTA 10 KWA MKUU WA MKOA WA DODOMA

Image
  Na; Happiness E. Chindiye        Habari - Dodoma RS Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule Leo Novemba 28,224 amepokea Kompyuta 10 kutoka Benki ya NMB Mkoani hapa, ikiwa ni sehemu ya Benki hiyo kurudisha kwa jamii (CSR). Kompyuta hizo zitatolewa kama motisha kwa walimu ambao Shule zao zimefanya vizuri kwenye matokeo ya mitihani  kwa shule za Msingi na Sekondari. Walioshiriki kushuhudia  makabidhiano hayo ni baadhi ya walimu kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma.   #keroyakowajibuwangu #Dodomafahariyawatanzania #mtiwangubirthdayyangu

Yas YATAMBULISHA HUDUMA ZAKE MKOA WA DODOMA

Image
Mkurugenzi wa Yas Kanda ya Kati Bw. Said Idd (kulia) akizungumza na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya katika ofisi ya Katibu Tawala huyo Jengo la Mkapa Jijini Dodoma, kutambulisha mabadiliko ya kampuni hiyo pamoja na kutambulisha huduma zake Uongozi wa Kampuni ya Yas (awali Tigo) Kanda ya kati ulipofika kuzungumza na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar Mmuya kutambulisha mabadiliko ya jina pamoja na kutambulisha huduma zake. Picha juu na chini, uongozi wa Kampuni ya Yas ukimkabidhi zawadi Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya baada ya kumaliza mazungumzo yaliyolenga kutambulisha jina jipya na huduma za kampuni hiyo ya mawasiliano.   Na. Hellen M. Minja,       Habari – DODOMA RS Uongozi wa Kampuni ya mawasiliano nchini, @Yas  umemtembea Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar Mmuya ofisini kwake jengo la Mkapa Jijini Dodoma leo Novemba 28, 2024 kwa lengo la kutambulisha mabadiliko yaliyotokea kwenye kampuni hiyo ambayo awali ilijulik...

RC SENYAMULE AHIMIZA WANADODOMA KUJITOKEZA KUPIGA KURA

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule akiwa kwenye foleni ya kupiga kura kwenye kituo cha Shule ya Msingi Dodoma Mlimani, Mtaa wa Salmini, Kata ya Tambukareli Jijini Dodoma leo Novemba 27, 2024 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule akitafuta jina lake kwenye orodha ya wapiga kura kwenye kituo cha Shule ya Msingi Dodoma Mlimani, Mtaa wa Salmini, Kata ya Tambukareli Jijini Dodoma. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule akijaza karatasi za kupigia kura yake wakati wa zoezi la kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaofanyika leo Novemba 27, 2024  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule akitimiza haki yake ya kidemokrasia kwa kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Mtaa wa Salmini, Kata ya Tambukareli Jijini Dodoma. Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya akipiga kura yake katika Mtaa wa Mathias, Kata ya Miyuji Jijini Dodoma kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaofanyika leo Novemba 27, 2024 Katib...

CCM YAHITIMISHA KAMPENI ZAKE KATIKA KATA YA MRIJO - CHEMBA

Image
Na. Hellen M. Minja,        Ha sobari – DODOMA RS Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, leo Novemba 26, 2024, kimehitimisha rasmi kampeni zake kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024 katika viwanja vya Kata ya Mrijo, Wilaya ya Chemba. Akizungumza na wananchi wa Kata hiyo wakati wa zoezi la kufunga Kampeni hizo, Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Gavu, aliyekuwa mgeni rasmi amesema; “Lazima tutulie sana na tufanye maamuzi yenye faraja na manufaa kwa ajili ya vizazi vyetu. Jukumu letu kwenu ni kuhitaji amani upendo na utulivu, jukumu la kuleta maendeleo tunalipenda. Chama chetu kina amini jukumu la uongozi ni kuwatumikia wananchi na si mtu mwenyewe” Ndugu Gavu Akitoa takwimu za idadi ya wagombea waliojitokeza na waliopitishwa na Chama hicho wakati wa mchakato wa kuwapata wagombea wa nafasi mbalimbali, Katibu wa CCM Mkoa Ndugu Pili Mbanga amesema; “CCM ilipata wagombea 29,447 ambapo wanaume ni 20,875 na wanawake ni 8,572. J...

MWAMKO WA WANAWAKE KUGOMBEA SERIKALI ZA MITAA WAONEKANA DODOMA

Image
Na. Hellen M. Minja,        Habari – DODOMA RS Wanawake wametajwa kuonesha mwamko mkubwa kwa kujitokeza kugombea nafasi za wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji, Mitaa pamoja na wajumbe wa Halmashauri za Vijiji /wajumbe wa kamati za mitaa ambapo wanawake 260 wamejitokeza kugombea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 Mkoa wa Dodoma. Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule alipokua akizungumza na waandishi wa Habari leo Novemba 26, 2024 katika ukumbi wa Ofisi yake, Jengo la Mkapa Jijini Dodoma kuutangazia Umma juu ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika kesho Novemba 27, 2024. “Katika ngazi ya Mitaa na Vijiji, wanawake 53 wamejitokeza kugombea nafasi za wenyeviti lakini katika ngazi ya vitongoji, wanawake 207 wamejitokeza kugombea nafasi hizo. Hii ni kuonesha kuwa angalau kumekua na mwamko sasa wa usawa wa kijinsia katika maeneo yetu”. Amesema Mhe. Senyamule. Aidha, ametaja baadhi ya majukumu ya wenyeviti wa Serikali za mitaa ...

RAIS AMEWEKA MAZINGIRA WEZESHI KWA WATU WENYE ULEMAVU.

Image
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule (Kushoto) akipokea Tuzo kutoka kwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na uratibu) Mhe. Ummy Nderiyananga kwa ajili ya kutambua ushiriki wake kwenye chakula cha pamoja na watu wenye ulemavu katika ukumbi wa Jakaya kikwete Conection Jijini Dodoma. Na; Sofia Remmi.        Habari - Dodoma RS Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,Bunge na Uratibu Ummy Nderiananga amempongeza  Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira wezeshi katika Sekta ya Elimu,ambayo lengo lake ni kuhakikisha watu wenye Ulemavu wanapata elimu bila vikwazo. Mhe. Nderiananga ameyasema hayo  leo Novemba 24, 2024 wakati wa hafla maalumu ya chakula cha pamoja na Watu wenye Ulemavu iliyoandaliwa na 'Tanzania Foundation For Excellence in Disabilities' (tfed). Akizungumza wakati wa hotuba yake,Mhe. Nderiananga Amesema kuwa Mhe. Rais ameendelea kutoa fedha kwa ajili ya kununua vifaa vya kujifunzia na kufundishia,sambamba  na kutoa...

DODOMA KUNA FURSA NYINGI ZA UWEKEZAJI,WAWEKEZAJI NJOONI MUWEKEZE : RC SENYAMULE

Image
  Na; Happiness E. Chindiye        Habari - Dodoma RS Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary S. Senyamule usiku wa tarehe 23.11.2024 ameshiriki uzinduzi wa 'LC Luxury Apartaments' mpya za kisasa zilizojengwa ndani ya Jiji la Dodoma.  Akizungumza na halaiki iliyojitokeza kwenye uzinduzi huo, Mhe. Senyamule ametoa wito kwa wawekezaji wengine kuja kuwekeza ndani ya Jiji hili, kwani kuna fursa nyingi ambazo zimeletwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan. “Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan tunampongeza kwa yote anayoyafanya ndani ya Mkoa wa Dodoma ya kutaka wageni wa hadhi zote wanaokuja kupata sehemu ya kupumzika kutokana shughuli zinazofanyika Jijini hapa, hivyo nitoe wito kwa  wawekezaji wengine kuja kuweza Dodoma” -Mhe. Senyamule  #kurayakosautiyako    #ujanjanikupigakura                 #dodomatukotayarikupigakura #mtiwangubirthdayyangu

"SERIKALI YETU INATAKA UCHAGUZI WA AMANI NA UTULIVU" - RC SENYAMULE

Image
Na; Happiness E. Chindiye  Habari - Dodoma RS  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule amesema Serikali inataka uchaguzi wa amani ,utulivu ,haki na demokrasia,na kwamba Serikali ya Mkoa imejipanga kuhakikisha maelekezo hayo yanafuatwa. Akizungumza na kundi la Vijana Novemba 23,2024 katika mashindano ya Mdahalo wa Vyuo uliofanyika kwenye ukumbi wa Jiji Mtumba, Mhe. Senyamule amesema, “ Serikali yetu inataka uchaguzi wa Amani na utulivu Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan mmemsikia mara zote anataka haki na demokrasia sisi kama Serikali ya Mkoa wa Dodoma tumejipanga kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa haki,amani na utulivu.Kwa kufanya hivyo, itatuongezea mshikamano,Utaifa wetu na umoja kama Watanzania”   Mashindando hayo ya Mdahalo wa vyuo yaliongozwa na mada ; Ukosefu wa Uzalendo miongoni mwa wananchi huchangia ushiriki hafifu wananchi katika uchaguzi. #kurayakosautiyako    #ujanjanikupigakura                 #dodom...