RC SENYAMULE ATATUA MGOGORO WA UJENZI WA SHULE KIDOKA - CHEMBA

Na. Hellen M. Minja, Habari – DODOMA RS Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule, leo Oktoba 31, 2024, ametatua mgogoro kati ya wananchi wa Kata ya Kidoka juu ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kata, kufuatia Wananchi wa vijiji viwili vya Kidoka na Pangalua vilivyoko katika kata ya Kidoka,Halmashauri ya wilaya ya Chemba, wote kutaka shule ijengwe kwenye vijiji vyao. Mkuu wa Mkoa huyo ametatua mgogoro huo wakati wa mkutano wa hadhara kwenye Kijiji cha Pangalua,mkutano ambao lengo lake ni kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili wakazi wa kata hiyo,ikiwemo eneo la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata. “Serikali imeona wote mna mahitaji ya shule, mabishano haya yanatokana na dhamira njema, japo inatuchelewesha kwani ilitakiwa kufanyiwa maamuzi ya haraka. Tumeamua shule zijengwe mbili, kwa maana ya Kidoka na Pangalua. Shule mbili zitajengwa, kila Kijiji kipate ya kwake” Amesema Mhe. Se...